You are currently viewing HARMONIZE AWAPA SOMO WANAUME, TAFUTENI HELA

HARMONIZE AWAPA SOMO WANAUME, TAFUTENI HELA

Msanii mkubwa wa muziki nchini Tanzania na CEO wa Lebo ya Konde Music amewashauri wanaume kutafuta hela ili kuboresha uhusiano kati yao na wapenzi wao.

Kwa mujibu wa Harmonize, hatua ya kuomba msamaha huwa rahisi zaidi wakati mwanaume anapomsapoti mpenzi wake kihela, Alishauri kwamba mwanaume anapaswa kutumia hela kumfanya mwanamke asahau makosa yake badala ya kumtumia jumbe nyingi za kuomba msamaha.

“Tafuta hela ukishakuwa nazo ndiyo utajua msamaha unaombwaje. Hizo SMS zako unamjazia WhatsApp unazidi kumuumiza na kumkumbusha machungu. Mfanye asahau babuu. Mpeleke katika dunia nyingine,” anasema Konde Boy Mjeshi.

Harmonize anasema hayo wiki chache tu baada ya kumwaga mamilioni ya pesa katika juhudi za kumuomba msamaha mpenzi wake, Kajala Masanja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke