You are currently viewing HARMONIZE AWATOLEA UVIVU WAANDAAJI WA TAMASHA LA AFRIKA MOJA KISA PICHA YA ERIC OMONDI

HARMONIZE AWATOLEA UVIVU WAANDAAJI WA TAMASHA LA AFRIKA MOJA KISA PICHA YA ERIC OMONDI

Mkali wa muziki wa Bongofleva Harmonize ameonesha wazi kutofurahishwa na poster ya tamasha la Afrika Moja linalotarajiwa kufanyika nchini, Aprili 30 mwaka huu.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Boss huyo wa Konde Gang ameeleza kwamba kitendo walichokifanya waandaaji wa tamasha hilo sio cha kiungwana kufuatia picha yake kuonekana kubwa huku picha ya mchekeshaji nyota nchini Eric Omondi ikiwa ndogo.

Harmonize ameeleza kuwa Omondi ni mkubwa kwake kiumri na kisanaa pia, huku akidai kuwa picha hiyo imewekwa kama Omondi anakuja kufanya usafi tu katika uwanja wa KICC ambapo tamasha hilo litafanyika.

Hata hivyo amewataka waandaaji wa tamasha hilo watengeneze poster nyingine ili aweze kupost kwenye uso wa ukurasa wake wa Instagram.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke