Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize ameweka wazi masuala ya umiliki wa wimbo wa “Omoyo Remix”.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize ambapo amesema hana umiliki wowote kwenye wimbo huo na mapato yote yanakwenda kwa Mchungaji Jane Misso.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” amesema licha ya kutumia gharama zake kwenye Audio na Video, hatachukua hata asilimia 1 kwenye wimbo huo.
Hata hivyo amesema lengo ni kumuona Jane Misso akiwa amerejesha furaha yake na kung’aa kwa baraka za Mungu