Staa wa Muziki wa Bongofleva Harmonize Hataki kupoa kwenye harakati za kuupeleka muziki wake kimataifa hii ni baada ya kumetangaza Tarehe atakayoachia Album yake Mpya.
Kupitia InstaStory yake kwenye mtandao wa Instagram Harmonize Ametangaza kuwa Ataachia Album yake Mpya Mei 20 Mwaka huu.
Mapema mwezi Februari mwaka huu harmonize alitangaza ujio wa High school Deluxe Album version, mara baada ya album yake ya high school kufanya vizuri mtandaoni.
Mfumo huo wa deluxe version’ hufanywa na msanii katika album husika kwa kuongeza baadhi ya remix, au nyimbo mpya.