Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize bado anaendelea kulilia penzi la mpenzi wake wa zamani Fridah Kajala mtandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza kumnunulia gari aina ya Range Rover Evoque yenye jina lake “Kajala 1” kwenye Number Plate.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mdomo” amechapisha sehemu ya video ikionesha gari hilo na kuandika maneno ya kuomba msamaha.
Konde ameitumia njia hiyo katika mchakato wake wa kuendelea kuomba msamaha kwa mrembo huyo huku akisema gari hiyo ni ya ndoto yake.
“Hatakama Zingekuwa KAJALA 1. mpaka 10. Haziwezi Kufuta Maumivu Niliyo Kusababishia wewe Pamoja Na Familia Haziwezi Badili Chochote Tulichopitia Nawala Haiwezi Kuwa Sababu Ya Kunirudia ila Hiii (1) Inaeleza Majuto Ya Yote Niliyo Kufanyia ..!!!! Ninacho omba Kwako ni Msamaha wa thati Ya Moyo Wako ..!!!! FRIDA wewe ni Mtu Wa Mungu Sanaa…!!!” Ameandika Harmonize.
Ameendelea kwa kusema “Unasali Pia Bila shaka Unatambua Hakuna Mkamilifu Hutokuja Kuanza Upya Mama You Know me Better COME BACK Usisahau Mimi ni Mtoto wa Masikini Mwenzio Tuu Nina Familia Wajomba Shangazi Wadogo Na Ndugu Kibao Masikini Ambao Nikifa Leo Ndio Watakao Nizika Ila Nimeona Wewe Ndo Unastahili HICHI Kidogo Changu 🙏”
“Natamani Ujue Kwamba Nakupenda Sana Narudia Tena Nisamehe Na Unipatie Nafasi Ya Mwisho I LOVE YOU TAKE ME BACK Nakumbuka Kuna Siku Ulisha Wahi Niambia Hii Ni MOJA YA GARI YA NDOTO YAKO PLEASE TAKE IT FROM ME I LOVE YOU ❤❤🌹🌹🥲🥲 THANKS MY BROTHER @royazdad Samahani Kwa Usumbufu 🙏🙏🙏 @ceekvr”