Mwanamuziki wa bongofleva Harmonize ametusanua huenda akaja na High school Deluxe Album version, mara baada ya album hiyo kufanya vizuri mtandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize ametangaza rasmi kuachia ‘Deluxe edition’ ya album hiyo iliyotoka Novemba 5 mwaka Jana ikiwa na nyimbo 20.
Aidha amesema mzigo huo utatoka baada ya video ya wimbo wa Bakhresa kufikisha VIEWS million 5 kwenye mtandao wa youtube.
Mfumo huo wa deluxe version’ hufanywa na msanii katika album husika kwa kuongeza baadhi ya remix, au nyimbo mpya ambapo harmonize ametaja kuiongeza ngoma ya Bakhresa ambayo kwa sasa inafanya vizuri.