Mwanamuziki na CEO wa Konde Gang Harmonize amejipta pabaya mara baada ya kukosolewa vikali na wadau mbalimbali wanaosimamia haki za watoto nchini Tanzania kufuatia kitendo chake cha kupanda stejini usiku na mtoto wake wa kike katika tamasha lake la Afro East Carnival lililofanyika wekeend hii iliyopita jijini Dar es salaam.
Kituo kimoja cha redio nchini Tanzania kimethibitisha kuwa msanii huyo kwa sasa anasakwa na mamlaka za Ustawi wa Jamii, kufuatia kitendo chake hicho cha kuambatana na kumpandisha mtoto mdogo katika tamasha lililofanyika usiku.