You are currently viewing HARMONIZE KUISHTAKI KAMPUNI YA UCHINA KWA TUHUMA ZA WIZI

HARMONIZE KUISHTAKI KAMPUNI YA UCHINA KWA TUHUMA ZA WIZI

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize amemtaka meneja wake Kajala Frida kuichukulia hatua za kisheria kampuni moja kutoka China ambayo inatengeneza cheni zenye chapa yake ya Konde Boy.

Kupitia Insta story yake kwenye mtandao wa Instagram, Harmonize ameeleza kwamba bila makubaliano yoyote, kampuni hiyo inatengeneza pesa kupitia chapa (brand) yake na inaziuza cheni hizo katika tovuti mtandaoni.

“Big brand in China. Am not getting any money out of it. Manager do something please @kajalafrida ” – ameandika Harmonize.

Aidha, madai ya namna hii yamekuwa yakitokea sana kwa mastaa kuhusiana na chapa zao kuigwa na kutengenezewa bidhaa na watu wengine bila makubaliano yoyote.

Sanjari na hilo amewapa utaratibu mpya mapromota wanapompatia show huku akiwataka wahakikishe kuna tiketi mbili za ndege daraja la juu (Business) ambapo moja yake na nyingine ya meneja wake Kajala. Pia ziwepo nyingine nane za kawaida (Economy) kwa timu yake na watu wa bendi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke