You are currently viewing HARMONIZE KUPOKEA GARI ALILOMNUNULIA EX WAKE IJUMAA HII

HARMONIZE KUPOKEA GARI ALILOMNUNULIA EX WAKE IJUMAA HII

Staa wa muziki kutoka nchini Tanzania Harmonize ameweka wazi kuwa siku ya Ijumaa atapokea gari jipya kutoka nchini Afrika Kusini aina ya Range Rover yenye rangi nyeusi kwa ajili ya aliyekuwa mpenzi wake Kajala Frida

Staa huyo amelithibitisha hilo kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram  kwa kuweka video ikionesha gari la kwanza aina (Range Rover) nyeupe alilotuonesha siku za nyuma na kusema amemnunulia mrembo huyo kama njia moja wapo ya kuendelea kumuomba msamaha.

Aidha amewatupia vijembe wakosoaji wake ambao wamekuwa wakimshutumu kwamba hana fedha za kutosha kununua magari ya kifahari kwa kusema kwamba anatumia suala hilo kutafuta kiki ili aendelee kuzungumzwa kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki.

Hata hivyo Harmonize ameahidi kuleta gari lingine lenye rangi nyeusi na atafanya ex-wake Frida Kajala kuwa na gari aina ya Range Rover mbili.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke