You are currently viewing Harmonize kutambulisha meneja na wasanii wapya Konde Gang

Harmonize kutambulisha meneja na wasanii wapya Konde Gang

Baada ya kuachana na aliyekuwa Meneja wake lakini pia mpenzi wake Kajala Frida , Msanii wa Bongofleva Harmonize ametangaza rasmi kutambulisha meneja wake mpya kama Suprise kwenye usiku wa Harmo-Night , show yake ya kufungia mwaka anayotarajia kuifanya siku ya tarehe 25 mwezi huu.

Kupitia insta story, Harmonize amefunguka kuutumia usiku huo pia kutambulisha wasanii wengine wapya kwenye lebo ya Konde Gang.

Lakini pia amedai kuwa ataitumia show yake ya Harmo Night 2022, kupima upendo na unafiki wa wasanii wenzie haswa aliofanya nao kazi ya pamoja na kuzalisha Hit songs.

Harmonize amesema kuwa endapo wasanii hao watashindwa kununua meza kuelekea show yake hiyo basi ndio utakuwa mwisho wa yeye kuongea nao huku akisisitiza kuwa hata kama msanii ana show nje ya Dar es salaam basi anunue meza na kualika watu wake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke