Huenda mwanamuziki Harmonize yupo mapenzini sasa baada ya muda kupita bila ya kuweka wazi hali ya mahusiano yake kwa sasa.
Hii ni kufuatia mfululizo wa post kutokea insta story yake kwenye mtandao wa Instagram zinazo ashiria kwamba huenda kwa sasa ameangukia kwenye penzi jipya na raia wa kigeni (mzungu) huku akiwa bado yupo nchini marekani.
Kupitia insta story yake Harmonize ameshare picha akiwa na mrembo wa kizungu na kuandika ujumbe unao tafsirika kwa maana ya “kumbukumbu iliyoje” ,jambo ambalo linahisiwa kuwa neno la fumbo kuhusu mahusiano yake kwa sasa.