Staa wa muziki kutoka nchini Tanzania Harmonize anataka kukibadilisha Kikohozi chake kuwa biashara.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Harmonize ametangaza kuja na bidhaa yake ya Sigara ambapo amewaomba mashabiki zake kumpa Jina zuri na kumsaidia kubuni muundo wa Sigara hizo.
Boi huyo wa Konde Gang Worldwide ametambua kuwa kwa hatua aliyofikia, si muziki wake pekee unaouza, bali ni jina lake ndilo lenye thamani zaidi ya kitu chochote kwa sasa. Kwa mtaji wa jina lake na wafuasi wake, anaweza kutengeneza fedha kubwa zaidi.