You are currently viewing HARMONIZE NA ALI KIBA WALAMBA DILI NONO LA UBALOZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM.

HARMONIZE NA ALI KIBA WALAMBA DILI NONO LA UBALOZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM.

Wasanii wa Bongofleva, Alikiba na ‘Harmonize wameteuliwa kuwa mabalozi wa ‘Safisha, Pendezesha’ Dar es Salaam, ukiwa ni mkakati wa usafi na uhifadhi wa mazingira mkoani humo.

Akizungumza katika hafla ya kunadhifisha jiji la Dar es Salaam,Ali Kiba amepongeza shughuli ya kuwahamisha wafanyabiashara kuhusu usafi ilivyofanyika na kuwataka wajue kwamba serikali ya Tanzania ina nia nzuri kwani hata wateja wenyewe wanataka kupata huduma katika sehemu iliyo safi.

Hitmaker huyo wa “Bwana Mdogo” amesema kama balozi, anawahamasisha watu kuzingatia usafi na kuwa kama nchi za mbele ambazo ukipita unaona hata aibu kutupa taka na kuongeza kuwa hata yeye anaamini asingekuwa msafi watu wasingempenda.

Kwa upande wake, Bosi wa lebo ya muziki ya Konde Gang Harmonize amesema anafurahi kuwa balozi, na atahakikisha anatumia nafasi yake kuifanya Dar es Salaam inakuwa safi,huku akitamani kuiona inakuwa kama nchi ya Australia.

Utakumbuka mkakati wa kunadhifisha jiji la Dar es Salaam  unakuja mara baada ya kufanyika kwa shughuli ya kuwahamisha wachuuzi katika maeneo yasiyo rasmi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke