You are currently viewing HARMONIZE & OTILE BROWN KUJA NA EP YA PAMOJA YENYE NYIMBO 5

HARMONIZE & OTILE BROWN KUJA NA EP YA PAMOJA YENYE NYIMBO 5

Nyota wa muziki wa Bongofleva Harmonize ametangaza ujio wa EP ya pamoja mkali wa muziki nchini Otile Brown.

Harmonize ameweka wazi hilo akiwa jukwaani kwenye tamasha la Afro Vasha Disemba 12 mwaka huu huko Naivasha ambapo amesema EP hiyo itakuwa na Jumla ya mikwaju 5 ya moto.

Hajabainika kama EP hiyo ni ile Harmonize alituahidi atawashirikisha wasanii 5 wa Kenya wenye vipaji bila kuangalia ukubwa wa msanii ila ni jambo la kusubiriwa.

Ikumbukwe kabla ya Hitmaker huyo wa Teacher kutua nchini Kenya alidokeza mpango wa kufanya ziara ya kimuziki kwenye miji kumi za Kenya ambapo aliwapa nafasi mashabiki wapendekeze majina ya miji ambayo wangependa afanye tamasha lake la muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke