Msanii wa Rico Gang, Harry Crazee amefunguka tusiyoyajua kuhusu maisha yake kwa kusema kwamba karibu wanawake aliokuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi wamuharibie shughuli zake za muziki.
Katika mahojiano yake hivi karibuni amesema alijipata ameingia kwenye msongo wa mawazo na kuanza kubugia pombe kupindukia kutokana na shinikizo alizokuwa anapewa na wanawake aliokuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba jambo hilo lilimpekea kutaka kujiua mara tatu lakini hakufaulu kufanya hivyo baada ya watu wake wa karibu kumsaidia kimawazo.
Hata hivyo ametoa changamoto kwa vijana kuacha matumizi ya pombe na dawa za kulevya kwani ndio chanzo cha wao kuanza kuwa na mawazo ya kutaka kujitoa uhai kutokana na changamoto za maisha.
Harry Craze ni mmoja wa wasanii wanaounda kundi la Rico Gang akiwa pamoja na Triand Rands hii ni baada ya Graycee kujiondoa.