You are currently viewing HART THE BAND KUACHIA ALBUM YAO MPYA MWISHONI MWA JUMA HILI

HART THE BAND KUACHIA ALBUM YAO MPYA MWISHONI MWA JUMA HILI

Kundi la muziki nchini Hart the Band limetangaza rasmi kuachia album yao mpya mwishoni mwa juma hili.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa kundi hilo, limechapisha cover ya album yao kwa jina Party Time huku likisema album hiyo itatoka rasmi Mei 6 mwaka huu wa 2022.

Party time album ina nyimbo nane za moto ikiwa na kolabo 3 kutoka kwa wakali kama nyashinski, Alika na Phyl the kangogo.

Hii inaenda kuwa album ya tatu kutoka kwa Hart the Band baaada ya, ‘Made In The Streets‘iliyotoka mwaka 2019 na ‘Simple Man’ iliyotoka mwaka 2021.

Utakumbuka Hart The Band ni kundi la muziki kutoka Kenya na linaundwa na wasanii watatu ambao ni Mordecai Mwini Kimeu, Wachira Gatama, na Kenneth Muya Mukhwana.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke