Kundi la muziki nchini Hart the Band limeachia rasmi album yao mpya iliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki zao kwa muda.
Album hiyo inayokwenda kwa jina la Party time ina nyimbo nane za moto ikiwa na kolabo 3 kutoka kwa wakali kama nyashinski, Alika na Phyl the kangogo.
Party time album ina nyimbo kama Jienjoy, Na Bado, Sitaki Ma-Pressure, Easy like ABCD inapatikana exclusive kwenye digital forms zote za kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni ikiwemo Boomplay, Sportify, Hustle sasa na nyingine nyingiu.
Party time ni Album ya tatu kutoka kwa Hart the Band baaada ya, ‘Made In The Streets‘iliyotoka mwaka 2019 na ‘Simple Man’ iliyotoka mwaka 2021.
Utakumbuka Hart The Band ni kundi la muziki kutoka Kenya na linaundwa na wasanii watatu ambao ni Mordecai Mwini Kimeu, Wachira Gatama, na Kenneth Muya Mukhwana.