You are currently viewing HART THE BAND WAONYA VIJANA DHIDI YA KUBUGIA POMBE KUPINDUKIA

HART THE BAND WAONYA VIJANA DHIDI YA KUBUGIA POMBE KUPINDUKIA

Wasanii wa kundi la Hart the band kutoka Kenya wamewaonya vijana dhidi ya kubugia pombe kupindukia.

Wakizungumza moja kwa moja na Mpasho, wamesema vijana siku hizi wamekuwa waraibu wa kutumia vileo bila kuchukua tahadhari, jambo ambalo wamedai kuwa ni tishio kwa usalama wao ikizingatiwa kuwa wengi usahau kula na hata kuendesha magari kiholela wakiwa walevi.

Katika hatua nyingine wamesema hawatumii ‘kiki’ kutambulisha kazi zao za muziki kwa sababu si aina ya maisha ambayo wamezoea tangu waanze muziki miaka kumi iliyopita.

Wasanii hao ambao walilamba dili la ubalozi wa kinywaji cha Black & White wameongeza kuwa aina ya mashabiki wao pamoja na kazi zao nzuri za muziki wanazotoa pia huwafanya wasifikirie kabisa masuala ya kiki kama ambavyo hufanyika kwa baadhi ya wasanii hapa nchini Kenya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke