You are currently viewing HIGH SCHOOL ALBUM YA HARMONIZE YAWEKA REKODI APPLE MUSIC NA AUDIO MACK

HIGH SCHOOL ALBUM YA HARMONIZE YAWEKA REKODI APPLE MUSIC NA AUDIO MACK

Ikiwa bado haijatimiza wiki moja, album mpya ya msanii wa Bongofleva Harmonize  iitwayo “High School” imejiwekea rekodi ya aina yake kupitia Apple Music.

Tangu iachiwe Novemba 5, Album hiyo imefanikiwa kuchumpa na kuingia kwenye Top albums za mtandao wa apple music Tanzania.

Album hiyo yenye jumla ya mikwaju 20 ya moto, imekamata namba moja huku ikiiacha nafasi tatu album ya Ed Sheeran ‘Equals’. Na ya pili anaikamata Ali Kiba na album yake  ya ‘Only One King’ na nafasi ya nne imekaa EP ya mtu mzima Rayvanny, ‘New Chui’.

Lakini pia “High School” album imefanikiwa kupata streams zaidi ya Milioni Moja kwenye mtandao wa Audiomack pekee ndani ya siku mbili toka kuachiwa kwake.

Harmonize ambaye ni mkurugenzi wa lebo ya Konde Gang, kwa sasa anashikilia rekodi hiyo Apple Music na Audio Mack, na hili linadhihirisha kuwa “High School” inaendelea kufanya vizuri kupitia Digital Platforms mbalimbali za kupakua na kusikiliza muziki Duniani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke