You are currently viewing HITMAKER WA “MAPEPO” VISITA AFILISIKA KIUCHUMI, AOMBA MSAADA KWA WAHISANI.

HITMAKER WA “MAPEPO” VISITA AFILISIKA KIUCHUMI, AOMBA MSAADA KWA WAHISANI.

Msanii tajika nchini Visita ametoa wito kwa wahisani kumsaidia kifedha kwani amefilisika kiuchumi na hana mahala pakuishi.

Akiwa kwenye moja ya interview visita amesema kwa sasa anaishi kwenye studio ya kurekodia muziki inayomilikiwa na rafiki yake mmoja.

Hitmaker huyo wa Mapepo amesema alifurushwa kwenye  nyumba aliyokuwa akiishi kutokana na malimbikizi ya kodi aliyokuwa akidaiwa.

Mwezi Mei mwaka huu rapa huyo alichangiwa pesa na wasanii wenzake pamoja na marafiki mara  baada ya kushindwa kulipa gharama ya matibabu alipokuwa amelezwa hospitalini.

Visita ni moja kati ya wasanii walioacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini na anafahamika na hits kama Mapepo,Dawa ya moto, Dumbala Remix, Hivo ndio Kunaendanga, Fimbo na nyingine kibao.

Ikumbukwe tangu ujio wa msala wa corona wasanii wengi  nchini wameathirika kiuchumi na kimawazo baada ya kufungiwa matamasha ya muziki ambayo wamekuwa wakitegemea kuchuma riziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke