You are currently viewing Holy Dave akanusha tuhuma za kumshambulia mtu kwa chupa ya pombe

Holy Dave akanusha tuhuma za kumshambulia mtu kwa chupa ya pombe

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Holy Dave amekanusha madai ya kumjeruhi mtu kwa chupa ya pombe kwenye moja ya klabu ya usiku huko Kilimani, Nairobi.

Akimjibu shabiki yake aliyemtupia maneno makali mtandaoni baada ya kutajwa kuhusika kwenye kashfa hiyo, Holy Dave amesema ameshangazwa na namna watu wanavyomhukumu bila kujua undani wa taarifa hiyo.

Mwanamuziki huyo amesema madai ya kumpiga mtu na chupa hayana msingi wowote huku akisisitiza kuwa ukweli utabainika hivi karibuni.

“Don’t be too quick to judge. There was no beer bottle or any bottle involved. The truth will come out,” Alisema Holy Dave.

Wiki moja iliyopita Holy Dave alifikishwa katika mahakama ya Kibera kujibu mashtaka yaliyoibuliwa dhidi yake ya kumjeruhi, jamaa aitwaye Keem David na chupa ya pombe, akimuacha majeraha mabaya mwilini.

Hata hivyo alikana mashtaka yote mbele ya mahakama ambapo aliachiwa huru kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha ugomvi wao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke