You are currently viewing HUDDAH AMCHANA RIHANNA NA WANAWAKE WANAOWAKIMBIA WATOTO KWA AJILI YA STAREHE

HUDDAH AMCHANA RIHANNA NA WANAWAKE WANAOWAKIMBIA WATOTO KWA AJILI YA STAREHE

Mwanamitindo na mjarisimali Huddah Monroe amemtolea mvivu mwanamuziki kutoka marekani Rihanna baada ya video kusamba mtandaoni akiwa anakula bata kwenye moja ya show ya baba ya mtoto wake Asap rocky.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Huddah ambaye hana uhusiano mzuri na bosi huyo wa Fenty Beuaty ameonekana kuchukizwa na hatua ya rihanna kumtekeleza mtoto wake na kwenda kujivinjari ambapo ameenda mbali zaidi na kudai kuwa mastaa wengi hawajali watoo wao na ndio maana wengine wao wanapojifungua huwatelekeza watoto na kurudi  tena kwenye vilabu vya usiku.

“What is the pressure on women to be outside when nursing? Isn’t the baby more important? Help me understand” Amedai.

“Many have kids they don’t want just to use later as social media accessories that’s why they don’t care about their little ones…Coz chile, the way people give birth and run to the club is shocking. Have kids when ready! They will need you!” Ameongeza.

Kauli yaHuddah Monore’s imekuja wiki kadhaa baada ya kuwakosoa wana mitandao maarufu wa kenya kwa hatua kusapoti bidhaa za urembo za rihanna ambazo zilizinduliwa hapa kenya huku wakisusia kutangaza bidhaa za urembo za Huddah.

Rihanna pamoja na Asap Rocky walibarikiwa na mtoto mapema mwezi mei mwaka huu. Wawili hao kwa mara ya kwanza waliweka wazi taarifa njema kwa mashabiki zao kuwa wanatarajia kupata mtoto mwezi januari mwaka huu baada ya picha zao kusambaa  mtandaoni wakiwa huko Harlem Neywork city ambako Asap Rocky alizaliwa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke