Mrembo maarufu nchini, Huddah Monroe amedokeza kwamba hivi karibuni ataandika kitabu chake ambacho kitawasaidia watu kuhusu biashara.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kwamba kitabu hicho kitakuwa na masomo ya kutosha kuhusu jinsi ya kufanikiwa kibiashara na aliwahakikishia mashabiki wake kuwa watapenda kile ambacho atazungumza.
“Siku moja nitaandika kitabu changu cha biashara, mtajua kuwa nachukia video, kwa hivyo maarifa yote utalazimika kupata kutoka kwenye kitabu sababu nitamwaga udaku mwingi kuhusu biashara na mahusiano ya kibiashara” amesema Huddah Monroe.
Katika hatua nyingine, hivi karibuni, Huddah amekuwa akionekana kutokuwa sawa kiakili na mpaka kudokeza kuwa hayuko katika hali yake ya kawaida.
Hii ni baada ya madai kuwa mwanasosholaiti huyo ni mjamzito kufuatia picha aliyopakia Instagram, madai ambayo alijitokeza kukana na kusema umbo la tumbo lilisababishwa na nguo kubwa aliyokuwa amevaa.