You are currently viewing HUDDAH: SIJAWAHI KUWA SINGLE MAISHANI MWANGU

HUDDAH: SIJAWAHI KUWA SINGLE MAISHANI MWANGU

Mrembo maarufu nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, Huddah Monroe anaendelea kufunguka tusioysajua kuhusu maisha yake.

Kupitia instastory yake mrembo huyo amesema hajawahi kuwa single katika maisha yake yaani kwake kukaa bila mwanaume ni mwiko!

“Jambo la kwanza siwezi kaa bila mwanamume, wanaume wameninunulia magari na manyumba sijawahi kuwa single maishani mwangu sijui huwa wanafanyaaje kuuwa mtu kama mimi,” amesema Huddah.

Kauli yake inakuja siku chache baada ya kutusanua kwamba aliwahi kuolewa akiwa na umri wa miaka 19 na mwanamume ambaye hajamtaja jina lake.

Hata hivyo, hawakupata watoto kwa sababu mwanaume wake alikuwa mraibu wa dawa za kulevya.

“Nilikuwa kwenye ndoa (19), hatukuwa na mtoto na tukaachana kwa sababu mwanaume alikuwa mlevi wa dawa za kulevya! Sikuwa maarufu kwa hivyo sikuhitaji kuitangaza! So naongea kwa uzoefu. Si mzaha nyinyi nyote! Usiku mwema! Hiyo ndiyo siri yangu kubwa.” aliandika Insta Story.

Utakumbuka Huddah Monroe anahusishwa kuwa na mahusiano na Staa wa Bongofleva, Jux baada ya hivi karibuni kuonekana pamoja hadi kutokea kwenye video ya mwimbaji huyo, Sikuachi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke