Ubalozi wa Tanzania huko nchini Italia umempa shavu mwanamuziki Hussein Machozi ambaye anaishi nchini humo, kutoa burudani kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya Kiswahili, mjini Rome Italia Julai 7, mwaka huu.
Hussein Machozi ambaye anajulikana kwa ngoma zake kama “Kwa ajili yako”, “Hello”, “Addicted”, “Utaipenda”, “Unanifaa”, “Hoi” na nyingine nyingi, ametajwa kama mwanamuziki atakayenogesha siku hiyo kwa burudani ambapo hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Utakumbuka, Kiswahili tayari kinatambulika kama miongoni mwa lugha rasmi kwenye Muungano wa Afrika, na kinatumika kama lugha rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na bunge la Afrika na ni moja ya lugha za Afrika zinazozungumzwa na watu wengi duniani