Msanii wa Bongofleva Ibraah ameanika hadharani tracklist ya Album yake mpya inayokwenda kwa jina la King of New School.
Kupitia Instagram yake msanii huyo amechapisha artwork ya Album hiyo ambayo ina jumla ya ngoma 17 ya moto huku ikiwa na kolabo 6 pekee.
Ibraah amewashirikisha wakali kama AY, LAX, Christian Bella, Maud Elka, Bracket, Roberto huku Album yenyewe ikiwa na nyimbo kama Usiku mwema, Maumivu, body na nyingine nyingi.
Hata hivyo hajataja tarehe rasmi ya kuiachia album hiyo zaidi ya kuwataka mashabiki kuendelea kusalia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi.
King of New School ni album ya kwanza kwa mtu mzima Ibraah kuitoa tangu aanze safari yake ya muziki.