Msanii wa bongofleva Ibraah amejibu kuhusiana na tuhuma za kumtelekeza mtoto aliyezaa na Mrembo aitwaye Clyna aka Sugar ambaye amekuwa akijitokeza kwa mara nyingi mtandaoni tena kudai pesa ya matunzo ya mtoto wake wa kiume ambaye anadai amezaa na msanii huyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ibraah ameandika waraka mrefu huku akiambatanisha na picha ya mwanamke huyo pamoja na mtoto wake ambapo amekiri ni kweli alishawahi kuwa na ukaribu na mama wa mtoto huyo na yupo tayari kwa ajili ya vipimo (DNA) ili kuthibitisha kama kweli mtoto ni wake.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Ibraa ameeleza, “Taarifa zimenifikia kwasababu mama mzazi au muhusika mkuu amenihusisha na amesema yawezekana mimi ndio mwenye bahati hii ya mtende na nimeona nipost hapa ili kuondoa dhana na maneno yanayoendelea mitandaoni au ile hofu ya kwamba pengine naweza kuwa mjinga hadi ikafikia kuitelekeza damu yangu, kitu ambacho hakiwezekani na hakitokuja wezekana.
“Ni wazi kwamba mama mtoto alikuwa rafiki yangu siku za nyuma hilo halina siri na ndio maana sikusitushwa sana na hizi taarifa kama binadamu wa kawaida. Nitafata taratibu zote kwa kushirikiana na uongozi wangu pamoja na familia yangu kujihakikishia kwamba hii ni kweli damu ya Mtwara ili taratibu zingine ziendelee. Itakuwa faraja kubwa kwangu pale VIPIMO (DNA) vitakavyosema Yes huyu ni Chinga maana nitakuwa nimeshapata mwenzangu wakushirikiana nae katika safari hii ya kitendawili cha DUNIA.
“Niwaahidi tu hata kama ikitokea bahati mbaya vipimo vikatoa majibu tofauti na tunayo yatarajia basi still nitakuwa rafiki bora wa malaika mtukufu ili na yeye aonje utamu wa Dunia bila masemango au kubaguliwa kwani yeye hahusiki na hajui chochote zaidi ya kuzaliwa na anategemea sisi sote tumfanye mwenye furaha” – @ibraah_tz