Rapa Iggy Azalea amekanusha kuwa kwenye bifu na Nicki Minaj, Iggy ameibuka na kujibu shutuma hizo kufuatia Tweet ya New York Post ambayo ilianika wasanii wa Kike ambao wamewahi kuwa kwenye ugomvi na Nicki Minaj akiwemo Cardi B, Mariah Carey na Miley Cyrus.
Iggy alishuka kwenye comment na kukanusha hilo kwa kusema kwanini amewekwa kwenye orodha hiyo wakati anaamini pamoja hawajahi kusemeana vibaya.
Fahamu kwamba wawili hao walianza kuhusishwa kuwa kwenye bifu mwaka 2014 baada ya hotuba ya Nicki Minaj wakati akipokea Tuzo ya BET kutafsiriwa kuwa alimtolea uvivu mkali huyo wa ngoma ya “Fancy”.