Disemba mwaka huu, Instagram itafuta app ya “Threads for Instagram” ambayo ilianzishwa Mwaka 2019 ili kushindana na Snapchat.
Instagram imesema mwisho wa mwaka huu itafuta app ya Threads katika App Store na Google Play Store; na itakuwa haipatikani kwa watumiaji wote ambao bado wanaitumia.
Threads ni App ambayo Instagram ilianzisha ili kushindana na soko la Snapchat. Inafanana na Snapchat, inawezesha watumiaji kurekodi videos fupi na picha; pia inawezesha mtu kuchat na marafiki wa Instagram. Inaonekana watumiaji wengi hawakuipenda hii idea ya Instagram!