Kufuatia taharuki ambayo imekuwa ikijitokeza kwa watumiaji pale ambapo mtandao wa Instagram unakuwa umekumbwa na matatizo ya kiufundi, sasa mtandao huo umeanza majaribio ya ‘feature’ mpya ambayo itakuwa ikitoa taarifa pale linapojitokeza tatizo hilo.
Taarifa hiyo itakuwa ikitokea kwa mfumo wa notification kwenye ukurasa wa mtumiaji wa mtandao huo kumjulisha kuwa limejitokeza tatizo la kiufundi.