Kampuni ya Meta itachelewa kuweka mfumo wa Encryption katika chats za Instagram na Facebook Messenger mpaka mwaka 2023.
Kwa sasa ni WhatsApp tu ndio inatumia usalama wa End-to-End Encryption (E2EE), ambao ni mfumo wa kuongeza usalama katika chats. Katika mfumo huu wa E2EE ni mtumaji na mpokeaji ndio ambao wanaweza kusoma messages na chats. Inazuia Facebook (Meta), third-parties na mtu yoyote kuona chats.
Antigone Davis ambaye ni mkuu wa Kitengo cha Usalama cha Meta, amesema Meta itachelewa kuweka mfumo huo ili kuwa na uwezo wa kuendelea kudhibiti waovu au vikundi ambavyo vinatumia mitandao vibaya.