You are currently viewing Instagram yaweka sehemu mpya ya “Notes”.

Instagram yaweka sehemu mpya ya “Notes”.

Mtandao wa Instagram unazidi kuboresha huduma zake kwa kuweka sehemu mpya ya “Notes”

Sehemu hii inawezesha mtumiaji kuandika ujumbe mfupi usiozidi herufi 60. Ujumbe huo unaonekana upande wa juu sehemu ya DM, sehemu hii mpya itasaidia mtumiaji kuandika ujumbe mfupi kwa kutumia maandishi na emoji.

Notes zitakuwa zinakaa kwa masaa 24 na kufutika, ni sawa na Instagram Stories lakini ni kwa mfumo wa maandishi tu.

Sehemu hii mpya itakuwa inasaidia watumiaji kuandika mawazo yao au ujumbe mfupi wa kuwajulisha marafiki au watu wa karibu ambao unawasiliana nao kwenye DMs.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke