You are currently viewing INSTAGRAM YAWEKA UTARATIBU WA KUHAKIKI UMRI WA WATUMIAJI WAKE

INSTAGRAM YAWEKA UTARATIBU WA KUHAKIKI UMRI WA WATUMIAJI WAKE

Instagram ni app ambayo inataka watumiaji wote wawe na umri wa miaka 13 na kuendelea. Akaunti za watoto ambao wana umri chini ya hapo zitakuja kudhibitiwa.

Instagram ina utaratibu maalum kwa watumiaji wa Miaka 13 mpaka 17: Akaunti zao ni lazima ziwe Private na hazina matangazo. Kampuni ya Meta imetoa ufafanuzi kuhusu utaratibu mpya wa kuhakiki umri wa watumiaji.

Katika utaratibu mpya ambao umeanza kwa baadhi ya nchi, watumiaji watalazimika kuthibitisha umri kwa kujipiga Video ya Selfie huku ukiwa unageuka pande zote kuonyesha uso wako. Kisha baada ya kuchukua video ya selfie, utaituma Instagram na itakaguliwa kuthibitisha umri wako. Majibu ya kuthibitisha umri wako yanatoka kuanzia baada ya dakika 20.

Instagram imeshirikiana na kampuni ya Yoti; ambayo ni kampuni kubwa duniani inayohusika na kuhakiki umri na details za mtu kwa kutumia picha. mfumo wake unakagua bila kufahamu picha ya mtu, bila kuhifadhi picha ambazo zinahakikiwa na safe katika kutunza data zake.

Hatua nyingine ni kupiga picha kitambulisho au cheti za kuzaliwa. Na njia nyingine ni Vouching; ambapo unaweza kuomba mtu mzima athibitishe kuwa wewe ni mtoto. Akaunti ya mtu anayethibitisha hairuhusiwi kuthibitisha mtu zaidi ya mmoja

 

 

 

 

 

 

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke