Msanii nyota kutoka Uganda Irene Ntale amesema hana mpango tena wa kujiunga na lebo yeyote ya muziki kwa ajili ya kusimamia kazi zake.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Ntale amesema ameelekeza nguvu zake kufanya muziki kama msanii wa kujitegemea kwa kuwa inalipa sana tofauti na lebo za muziki ambazo amezitaja kuwa zinapora pesa za wasanii.
Hitmaker huyo “Onkubirako” amesema hajutii kusainiwa na lebo ya muziki Universal Music Africa ikizingatiwa kuwa ilitimiza ahadi zote walizompa kwenye muziki wake.
Utakumbuka Irene ntale alikuwa amesainiwa kwenye lebo ya muziki ya Swangz Avenue kabla ya kujiunga na kampuni ya Universal Music Group ambayo aliigura mwaka wa 2020.