Staa wa muziki nchini Uganda Irene Ntale amekuwa akisema kwamba yupo tayari kwa ajili ya ndoa na iwapo hilo litatimia anataka kuolewa na mwanaume wa ndoto yake. Lakini inaonekana mrembo huyo anafuatwa na vijana wadogo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Irene Ntale amesema hayuko tayari kuchumbiana na vijana wadogo ambapo ametoa onyo kwao kuacha tabia ya kumsumbua kwenye mitandao yake ya kijamii kama hawajafikisha umri wa miaka 30.
Ikumbukwe Irene ntale amekuwa akisumbuka kumpata mwanaume atakayemuoa tangu aachane na aliyekuwa mchumba wake Jonathan Kyeyo. Jambo hilo lilimlazimu kutangaza kwamba yupo singo na hilo limepelekea wanaume wa kila aina kuanza kumchumbia.