You are currently viewing IRENE NTALE AWATAKA MASHABIKI WAMTAFUTIE MUME

IRENE NTALE AWATAKA MASHABIKI WAMTAFUTIE MUME

Mwanamuziki kutoka Uganda Irene Ntale hana mpenzi anayefahamika kwa muda mrefu.

Baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Jonathan Kyeyo, Ntale amekuwa akihangaika kutafuta mwanaume sahihi.

Irene Ntale ambaye amekata tamaa sasa kwenye suala la kutafuta mume wa ndoto yake, amewapa mashabiki wake jukumu la kupendekeza mwanamume  atakayemuoa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “Kwa kuwa nyinyi watu mnataka niolewe vibaya sana na hamwezi kuniruhusu nipumue, pendekeza mume anayefaa kwenye mitaa hii ya Twitter,”

Hii si mara ya kwanza kwa Irene Ntale kupeleka matatizo yake ya mahusiano ya kimapenzi kwa mashabiki wake.

Hapo awali, aliwauliza wafuasi wakekwenye mitandao ya kijamii ni kwa nini wanaume wachanga wanaogopa kumchumbia kwa ajili ya mapenzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke