You are currently viewing IRYN NAMUBIRU AKANUSHA TUHUMA ZA KUMUBURUZA MAHAKAMANI MAMA YAKE MZAZI

IRYN NAMUBIRU AKANUSHA TUHUMA ZA KUMUBURUZA MAHAKAMANI MAMA YAKE MZAZI

Msanii nyota kutoka nchini Uganda Iryn Namubiru amekanusha tuhuma za kumfungulia mashtaka mama yake mzazi kutokana na mzozo wa ardhi unaondelea kati yao.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Iryn Namubiru amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwani mama yake huyo amekuwa akimzushia tuhuma za uongo kwa muda sasa kwa lengo la kusambaratisha juhudi zake za kumzuia asiuze ardhi ya familia.

Msanii huyo amewataka wanaoeneza taarifa hizo zinazoibuliwa na mama yake wakome mara moja huku mashabiki wakimtaka akae mbali na mama yake mzazi ili kuepuka ugomvi uliopo kati yao kama kweli anataka kushinda kesi ya ardhi dhidi yake.

Kauli ya Iryn Namubiru imekuja mara baada ya kudaiwa kuwa alikamatwa mapema wiki kwa madai ya kumtishia maisha mama yake mzazi kutokana na mzozo wa ardhi.

Utakumbukwa kwa miaka kadhaa sasa Iryn Namubiri pamoja na mama yake mzazi wamekuwa wakigombania kipande cha ardhi kilichoachwa na babu yake mwaka wa 1998 alipofariki duniani huko Nambale, Mityana nchini Uganda.

Mwaka  wa 2021 Iryn aliibuka na kudai maisha yake yamo hatarini kutoka na mzozo wa ardhi kati yake na mama yake mzazi ambapo alienda mbali zaidi na kusema kuwa chochote cha weza kutokea kwani mama yake anaweza tupwa jela.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke