Msanii wa lebo ya Utembe World, Iyanii ametetea hatua yake ya kuwa nusu uchi kwenye hafla ya uzinduzi wa album mpya ya bosi wake Arrow Boy.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Iyanii amesema aliahamua kufanya hivyo kama njia ya kuonyesha ubunifu kwenye masuala ya mitindo na fasheini kwani ni kitu ambacho amekuwa akifanya tangu utotoni.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Pombe” amekanusha kutumia suala hilo kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari nchini ikizingatiwa kwamba yeye ni moja kati ya wasanii wasiopenda kutumia kiki kutangaza muziki wake.
Utakukumbuka Iyanii ni moja kati ya wasaniii waliotumbuza kwenye hafla ya uzinduzi wa album ya Focus ya Arrow boy Usiku wa kuamkia Machi 13 Jijini Nairobi.