You are currently viewing Iyanii apokezwa tuzo mbili Boomplay baada ya kufikisha streams millioni 10

Iyanii apokezwa tuzo mbili Boomplay baada ya kufikisha streams millioni 10

Mwanamuziki Iyanii kutoka nchini Kenya anaendeleza ubabe upande wa Streaming Platforms hasa katika mtandao wa Boomplay, amepokea tuzo mbili za (plaque) kutoka Boomplay baada ya ya kufikisha zaidi ya streams milioni 10 kupitia nyimbo zake zote zinazopatikana kwenye mtandao huo.

Iyaani ameamua ku-share plaque kutoka Boomplay kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kufikia kiwango hicho ambapo amewashukuru mashabiki wake kwa upendo wanaoendelea kumuonyesha bila kuchoka kwenye muziki wake.

Katika hatua nyingine Wimbo wake “Pombe”, umefanikiwa kufikisha zaidi ya streams milioni 5 kwenye mtandao wa Boomplay.

Wimbo huo, ulitoka rasmi mwaka 2021 chini ya lebo ya muziki ya Utembe World inayomilikiwa na Arrow Boy.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke