Rapa kutoka nchini Marekani Jack Harlow ameweka wazi kwamba ataanza kuwasainisha Wanawake mikataba maalum ya makubaliano kabla ya kuingia penzini.
Akizungumza na Jarida la GQ, Jack Harlow amesema itabidi mwanamke asaini makubaliano hayo (Non-disclosure agreement) kwa ajili ya kutoanika mtandaoni kitu chochote ambacho kitafanyika baina yao wakiwa kwenye mahusiano.
Jambo kama la ujumbe mfupi wa maandishi ambao watakuwa wakitumiana kwenye simu, ubaki kuwa siri kati yao na sio kwa ajili ya kwenda mitandaoni.
Aidha amesema mwanamke ambaye hatapenda kusaini mkataba huo, hatopata nafasi ya kuwa naye.