You are currently viewing Jacquiline Mengi agonga mwamba kesi ya mirathi

Jacquiline Mengi agonga mwamba kesi ya mirathi

Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe, wamekwama kutetea wosia ulioachwa na marehemu baada ya Mahakama ya Rufani kutupa shauri lake la kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu.

Jacquiline alifungua shauri mahakamani hapo la mapitio kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu, iliyokataa wosia uliodaiwa kuachwa na Mengi.

Shauri hilo la mirathi namba 39 ya mwaka 2019, lilifunguliwa na watu wanne, wakiwemo ndugu wa marehemu Mengi.

Mahakama hiyo katika uamuzi wake uliotolewa juzi na jopo la majaji watatu, Rehema Mkuye (kiongozi), Dk Paul Kihwelu na Panterine Kente lilitupa shauri hilo kutokana na kasoro mbili zilizoonekana kwenye kiapo cha Jacquiline na cha wakili wake, Audax Kahendaguza vilivyoambatanishwa katika maombi hayo.

Kasoro hizo ambazo mahakama imekubaliana nazo ni viapo kuwa na maelezo yasiyopaswa kuwemo kwa hoja zinazohitaji ushahidi, maoni, mapendekezo na hitimisho na nyingine ni kutokubainisha chanzo cha taarifa ziliozokuwemo kwenye viapo hivyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke