You are currently viewing JAGUAR AGEUKIA MUZIKI BAADA YA KUSHINDWA NA SIASA

JAGUAR AGEUKIA MUZIKI BAADA YA KUSHINDWA NA SIASA

Aliyekuwa Mbunge wa Starehe Charles Njagua, almaarufu Jaguar amerejea rasmi kazi yake ya muziki baada ya kushindwa kutetea kiti chake cha Ubunge.

Jaguar, ambaye anasherehekewa na wengi kutokana nyimbo zake kali alizozitoa kipindi cha nyuma, ameachia wimbo wake mpya uitwao “Nitume” ambao amemshirikisha msanii wa injili kutoka Uganda Ambassador.

“Nimeachia wimbo wangu mpya #Nitume baada ya mapumziko marefu. Nilishirikiana na kaka yangu @ambassadaofficial kutoka Uganda. Sasa Inapatikana YouTube (link kwenye bio),” aliandika Instagram.

Mapema kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, Jaguar alipinga uteuzi wa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Simon Mbugua kuiwakilisha chama cha UDA kwenye uchaguzi mkuu.

Jaguar ambaye aliingia kwenye mitandao ya kijamii kulalamikia zoezi hilo alieleza kuwa lilikuwa na dosari kwani wapiga kura wa Starehe walinyimwa nafasi ya kuchagua kiongozi wao.

Utakumbuka  mgombea wa Chama cha Jubilee Amos Mwago alishinda kiti cha Ubunge cha Starehe baada ya kushinda kwa kura 50,787 nyuma ya mpinzani wake Simon Mbugua wa Chama cha United Democratic Alliance (UDA) aliyepata kura 35,548.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke