You are currently viewing JAGUAR AKANUSHA KUMKIMBIA ERIC OMONDI WAKATI WA MAANDAMANO

JAGUAR AKANUSHA KUMKIMBIA ERIC OMONDI WAKATI WA MAANDAMANO

Mbunge wa Starehe Charles Njagua maarufu kama Jaguar amekanusha madai yanayotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa alidinda kusimama na Eric omondi mapema wiki hii alipokuwa anawasilisha bungeni mswada wa kuleta mabadiliko kwenye muziki wa Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari Jaguar ambaye ni mwanamuziki amesema yeye ndiye alimkingia kifua eric omondi hadi akaachiwa uhuru alipokamatwa na polisi katika majengo ya bunge.

Hata hivyo hitmaker huyo wa “Kigeugeu” amesema anaunga mkono mawazo ya eric Omondi ya kutaka asilimia 75 ya muziki zipigwe kwenye vituo vya redio na runinga nchini ila Omondi hakufuata njia sahihi ya kuwasilisha mswada huo bungeni.

Ikumbukwe kwa wiki moja  sasa eric omondi amekuwa akitoa changamoto kwa  wasanii wa Kenya kutia bidii kwenye kazi zao kwani muziki wa Kenya umeonekana kupoteza mweelekeo katika siku za hivi karibuni.

Hii ni baada ya wasanii wa mataifa mengine kuonekana kupewa kipau mbele kufanya shows nchini huku wasanii wa Kenya wakiwekwa pembeni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke