Bondia maarufu kutoka Marekani Jake Paul ametaka vita ya maneno inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii, kati ya rapa Kanye West na Pete Davidson kuhusu Kim Kardashian ifike mwisho.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 25 ametoa ofa ya shilling billioni 3.4 za Kenya kwa kila mmoja kupambana ulingoni ili kumaliza vita yao kwa mwanamama Kim Kardashian.
Jake Paul amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo ameeleza kuwa pesa hizo ataziweka ulingoni kabla ya raundi ya 6, huku nia yake ni kutaka bifu hilo liishe kiume kabla ya watoto hawajapata athari zaidi.
Kauli ya Jake Paul imekuja mara baada ya Kanye West kuonekana kumshambulia Pete mtandaoni akidai kuwa amekuwa kizingiti kwake kuwaona watoto wake