You are currently viewing JALANG’O AFUNGUKA KUHUSU ISHU YA KUTOKEA KWENYE VILABU VYA BURUDANI

JALANG’O AFUNGUKA KUHUSU ISHU YA KUTOKEA KWENYE VILABU VYA BURUDANI

Mtangazaji wa radio ambaye kwa sasa ni mbunge mteule wa Lang’at Felix Oduor maarufu Jalang’o amedokeza mpango kufanya kipindi cha asubuhi kwenye radio.

Katika kikao cha maswali na majibu kwenye Instagram Jalang’o amesema ana upendo kwa radio kwa kuwa ni chombo ambacho kimemfungulia milango nyingi katika maisha yake.

Hata hivyo mwanasiasa huyo amesema hatakuwa mshereheshaji kwenye maonyesho ya burudani  lakini pia hatatokea kwenye vilabu vya burudani kutokana na majukumu mengi ambayo yatakuwa yanamuandama kama mbunge wa Lang’at.

Utakumbuka jalango alimbwaga  mbunge wa langat anayeondoka Nixon Korir wa UDA kwenye uchaguzi mkuu uliokamilika majuzi nchini Kenya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke