You are currently viewing Jalang’o akanusha kutoka kimapenzi na Diana B

Jalang’o akanusha kutoka kimapenzi na Diana B

Mchekeshaji aliyegeùkia siasa Jalang’o amepuzilia mbali uvumi wa muda mrefu kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na mke wa Bahati, Diana B.

Kwenye mahojiano na Mungai Eve, Jalango ambaye ni mbunge wa Lang’ata amekanusha madai hayo kwa kusema kwamba uhusiano wake na Diana ulikuwa ni wa kirafiki tu.

Aidha amenyosha maelezo kuhusu picha inayosambaa mtandaoni akiwa na Diana kwa kusema kuwa alipiga picha hiyo na mama huyo wa watoto watatu takriban miaka 15 iliyopita alipokutana naye kwenye duka moja la jumla jijini Nairobi.

“I remember that photo must have been taken in 10-15 years old at Jamia mall. She requested for a photo and I took a photo with her. I have never dated Diana. Diana has been my friend for the longest time and even when we took that photo it was just a good photo.”, Alisema.

Kauli yake imekuja mara baada ya walimwengu kuhoji kuwa wawili hao walikuwa wapenzi kipindi cha nyuma kutokana na hatua ya Diana B kukiri hadharani kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na wanaume matajiri kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya msingi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke