Nyota wa muziki kutoka Marekani Janet Damita Jo Jackson maarufu kama Janet Jackson ambaye ni dada wa marehemu Michael Jackson, ametangaza uzinduzi wa pili wa album yake iitwayo ”The Velvet Rope”.
Kampuni ya Universal Music Group pia imethibitisha hilo na kueleza kwamba album hiyo ambayo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza Oktoba 7 mwaka 1997, itazinduliwa tena Ijumaa hii, Oktoba 7 mwaka 2022 ikiwa ni miaka 25 tangu uzinduzi wa kwanza.
Kwenye album hiyo kutakuwepo na nyimbo zilizoimbwa upya na itapatikana kwenye majukwaa yote ya muziki mitandaoni. Pia fahamu, ”The Velvet Rope” ilikuwa ni album ya sita ya Janet Jackson.
Kwa msaada wa mtandao, Inaelezwa kwamba mauzo ya album hiyo kipindi hiko yalikuwa mengi sana kiasi cha kuorodheshwa kama “Triple Platinum” na ilikuwa namba moja kwenye Billboard 200.
Pia inaelezwa, Janet Jackson alikuwa akisumbuliwa na msongo wa mawazo kiasi ambacho aliamua kusimulia kupitia album yake hiyo “The Velvet Rope” mwaka 1997.