You are currently viewing JASON DERULO ATAJA SABABU YA MASHINDANO YA MUZIKI KUFELI KUTOA MASTAA

JASON DERULO ATAJA SABABU YA MASHINDANO YA MUZIKI KUFELI KUTOA MASTAA

Msanii nyota kutoka nchini Marekani Jason Derulo amefunguka sababu zinazofanya mashindano mengi ya uimbaji kushindwa kutoa Mastaa wenye uwezo wa kiushindani wanapoingia kwenye muziki.

Kwenye mahojiano na Billboard, Jason amesema mashindano mengi kama The Voice Chilevision na American Idol hushindwa kutoa Mastaa kwa sababu huzingatia sauti ya msanii pekee na kusahau vitu vya ziada.

Msanii huyo amemtolea mfano msanii Cardi B kuwa alipata umaarufu kabla hata ya kuanza kuimba kwa sababu alikuwa na vitu vya ziada.

“I think a lot of times in these competition-based shows, they’re not looking for a special thing about a person but they’re looking for the best voice. Unfortunately, that is not what makes a star. It’s a special something about somebody that makes a star,” Amesema Jason.

Ameongeza “Cardi B, before she put out any music, people were into Cardi B, she had that special something,”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke