Mwanamuziki wa Bongofleva Jay Melody ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake wa miondoko ya Amapiano “Acha Wivu “ameamua kufuta post zote kwenye ukurasa wake wa Instagram zinazohusiana na wimbo huo.
Mpaka sasa haijafamika sababu za Jay Melody kufuta post za wimbo huo japo stori za chini ya kapeti zinadai kuwa ni kutokana na wimbo huo kutopata mapokezi mazuri ukilinganisha na nyimbo za nyuma alizoziachia
Mpaka sasa wimbo huo umesikikizwa na watu 59,000 kupitia mtandao wa YouTube