You are currently viewing JAY MELODY AWEKA HISTORIA NA WIMBO WAKE “NAKUPENDA”

JAY MELODY AWEKA HISTORIA NA WIMBO WAKE “NAKUPENDA”

Staa wa muziki wa Bongofleva Jay melody anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na wimbo wake “Nakupenda” ambayo tayari ina takriban wiki tatu tangu itoke rasmi.

Habari njema kwa mashabiki wa Jay Melody, ni kwamba ngoma yake “Nakupenda”, imefanikiwa kufikisha jumla ya streams Milioni 10 ndani ya digital platforms zote ambazo wimbo huo umepandishwa.

Wimbo huo ambao bado hauna video, na kwenye Shazam unakamata nafasi ya 2 kwenye kipengele cha Afrobeats na ya 82 Worldwide.

Itakumbukwa, “Nakupenda” ni wimbo wa tatu kwa Jay Melody kuachia mwaka huu, baada ya “Sugar” pamoja na Remix yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke